Friday, January 11, 2013

STARS YAFUNGWA 2-1 ETHIOPIA KATIKA MCHEZO WA KIRAFIKI.
Taifa stars
Timu ya Ethiopia
Timu ya Taifa ya tza ‘Taifa Stars’ ilikuwa dimbani huko Addis Ababa, Ethiopia kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya wenyeji katika dimba la Taifa la Addis Ababa na matokea ni kwamba stars imefungwa mabao 2-1. Huku bao la kufutia machozi la stars likifungwa na mbwana samata.
Mchezo huo kati ya Stars na Ethiopia ulikuwa ni maandalizi ya mwisho kwa Ethiopia kabla ya kwenda Afrika Kusini kwenye fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), zitakazoanza Januari 19 mwaka huu.
Aidha, Stars  itautumia mchezo huo kama sehemu ya maandalizi ya mechi ya mchujo dhidi ya Morocco kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia 2014, mchezo utakaochezwa Machi mwaka huu. 
.

No comments: