![]() |
Didier Ddrogba |
Galatasaray walithibitisha Jumatau kuwa Drogba mwenye umri wa miaka 34 ameshakubali kusaini mkataba wa miezi 18 na klabu hiyo unaokadiriwa kufikia kiasi cha euro milioni sita huku kiasi euro milioni nne akikabidhiwa nyota huyo.
Hatahivyo Shenhua ambao walimsajili Drogba baada ya kuondoka Chelsea katika kipindi cha majira ya kiangazi msimu uliopita walionyesha kushangazwa na taarifa hizo na wameamua kulipeleka Shirikisho la Soka la Dunia-
FIFA ili lipate ufumbuzi. Kwasasa Drogba yuko ya timu yake ya taifa katika michuano ya Mataifa ya Afrika inayoendelea nchini Afrika Kusini huku timu yake ikiwa tayari imesonga mbele katika hatua ya robo fainali baada ya kushinda michezo yake miwili ya kwanza
No comments:
Post a Comment