Wednesday, January 30, 2013

NI IVORY COAST  NA TOGO NDIZO ZILIZOINGIA HATUA YA MTOANO KUNDI D, TUNISIA NA ALGERIA ZATUPWA NJE BAADA YA SARE KUTAWALA LEO KATIKA MICHUANO YA AFCON AFRIKA YA KUSINI

Ivory Coast imemaliza mechi zake katika kundi D kwa kuongoza ikiwa na pointi saba.

Matokeo hayo yanafuatia mechi zake mbili za awali kwa kushinda zote dhidi ya Togo na Tunisia na kutoka sare ya 2-2 na Algeria katika mchezo wa mwisho.

Timu ya Ivory Coast ilikuwa ikikamisha ratiba na kutafuta nafasi katika kundi hilo kwani ilikuwa imekwisha fuzu kucheza robo fainali
Algeria, nayo ilicheza mechi hiyo, ikiwa na uhakika kuwa matokeo ya mechi hiyo hayatakuwa na maana kwao, baada ya kuyaaga mashindano hayo, kwani ilikuwa imepoteza michezo yote miwili ya awali.


Algeria ilipoteza mechi zake mbili dhidi ya Togo na Tunisia. Hata hivyo imeweza kuambulia pointi moja.

Katika mechi nyingine ya kundi hilo D, Togo ilipambana na Tunisia mechi ambayo imemalizika kwa timu hizo kufungana goli 1-1.


Timu zilizofuzu kutoka kundi D ni Ivory Coast na Togo ambayo ilikuwa na pointti 4 kama Tunisia, lakini Tunisia ikifungwa magoli mengi.


Tunisia ilihitaji ushindi katika mechi hiyo ili ifuzu kwa raundi ijayo huku togo nikihitaji sare ya aina yoyote ili kufuzu kwa raundi ijayo.

Togo ilianza mechi hiyo kwa vishindo huku ikipata bao lake la kwanza kunako dakika ya 12 kupitia kwa mchezaji Serge Gakpe ambaye alipokea pasi nzuri kutoka kwa nahodha wa timu hiyo Emmanuel Adebayor.

Kunako dakika ya 30 Tunisia ilizawazisha kupitia mkwaju wa penalti baada ya mshambuliaji wake Walid Hichri kuangusha kwenye eneo la hatari na Dare Nibombe.

Emmanuel Adebayor alipoteza nafasi nzuri sana dakika za mwanzo mwanzo za mechi hiyo na kadri mechi inavyoendelea, ndivyo wachezaji wa Tunisia wanvyoendelea kuimarika.

Khaled Mouelhi, ndiye aliye tunukiwa jukumu hilo la kuupiga mkwaju huo na bila ya kusita akaupachika wavuni, na kwa mara nyingine kufufua matumaini ya Tunisia ya kufuzu kwa robo fainali.

Baada ya dakika za kwanza 45, timu hizo mbili zilitoshana nguvu.

Tunisia ilianza kipindi cha pili huku ikiwa na nguvu zaidi na nusura ifunge bao la pili lakini mshambuliaji wake Oussama Darragi aliangushwa na Vincent Bossou.

Tunisia wapa penalti lakini walikosa penalti hiyo baada kugonga mwamba wa pembeni na mpira kurudi uwanjani. 
Kocha wa Tunisia Sabi Trabelsi alifanya mabadiliko kadhaa ili kuongeza nguvu kikosi chake.

Kocha huyo alimuondoa mshambuliaji wake mmoja Wahbi Khazri na mahala pake kuchukuliwa na Zouheir Dhaouadi ambaye anaweza kuchezakucheza safu ya kati na ushambuliaji.

Dakika ya sabini na nane, Tunisia ilipoteza nafasi nzuri ya kufunga bao la pili, pale mchezaji wake alipopoteza kwaju wa penalti.

Wachezaji kadhaa wa Togo walipinga uamuzi huo wa refa hatua iliyopelea watatu kupewa kadi ya njano, Jonathan Ayite, nahodha Emmanuel Adebayor na kipa Kossi Agassa.

Tunisia, iliendeleza mashambulio yao dhidi ya Togo lakini juhudi zao ziligongwa mwamba na hivyo Togo kuandikisha historia ya kufuzu kwa robo fainali kwa mara ya kwanza.

Hatua ya robo fainali inapigwa siku ya tarehe 2 na 3 mwezi February.

Mechi ya kwanza itawakutanisha wenyeji Afrika ya kusini na Mali katika dimba la Durban, wakati wa mechi mechi ya pili itawakutanisha Ghana na Cape Verde katika dimba la Port Elizabeth.

Robo fainali ya pili itapigwa Juma pili kati ya Ivory Coast na Nigeria, na katika mechi nyingine iatawakutanisha Bukina faso na Togo.


No comments: