MTWARA KWALIPUKA, VURUGU ZILIANZA JANA MTWARA MJINI SASA ZAHAMIA MASASI, HABARI ZILIZOTUFIKIA HIVI PUNDE , NYUMBA YA MBUNGE MASASI NA OFISI ZA HALIMASHAURI ZACHOMWA MOTO MJINI MSASI.
![]() |
Diwani Chihako wa kata ya Chikongola ambaye fujo zilianzia nyumbani kwake |
![]() |
Polisi wakimkwida kijana ambaye jina lake halikupatikana mara moja |
![]() |
Polisi wakiwa doria |
![]() |
Polisi wakiwaingiza garini baadhi ya watu waliokamatwa jana |
![]() |
Jengo la mahakama ya mwanzo likiwaka moto |
![]() |
Mwandishi wa habari wa chanel ten Jonh Kasembe Akiwa amejeruhiwa kichwana katika ghasi hizo na kushonwa nyuzi 7 |
POLISI jana wamelazimika kupiga mabomu ya machozi kutwa nzima katika mji wa Mtwara yakianzia katika kata ya Chikongola, Manispaa ya Mtwara Mikindani kutawanya wananchi walioizingira nyumba ya diwani wa kata hiyo Mohamedi Chihako kwa madai ya kuwahifadhi wachawi ndani ya nyumba yake, huku mwandishi wa habari mmoja akiripotiwa kujeruhiwa.
Habari ambazo hazijathibitishwa na kamanda wa polisi mkoani hapa, Maria Nzuki zinadai kuwa majira ya saa 10 kasoro za jioni watu wanaodaiwa kuwa ni wanajeshi wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) waliingilia kati na kuanza kupambana na polisi, baada ya askari mwenzao mmoja kupata kichapo cha polisi.
Habari zilisemakuwa polisi walikuwa wanasaka nyumba hadi nyumba na kutembeza mkong’oto na ndipo ulipoangukia kwa mwanajeshi mmoja ambaye aliomba msaada kambini naaskari wenzake kuwasilikumsaidia ambapo walianza kupambana na polisi
Wananchi walitoa tuhuma hizo baada ya kukuta ungo ikiwa na tunguri ndani yake ambayo inadaiwa kuwa ni ndege ya wachawi uwanjani kwa Diwani wa kata ya Chikongola maeneo ya makabuli Msafa.
Wananchi walijikusanya nyumbani kwa diwani huyo na kumshinikiza awatoe wachawi nje ili waweze kuwadhibu, amri iliyopingwa na diwani huyo.
Kadri mda ulivyokwenda ndivyo wananchi walivyozidi kuongezeka na hatimaye kulijitokeza kundi la watu walioanza kutia vurugu, hali iliyomlazimu Chihako kuomba msaada wa polisi.
Mashuhuda wa tukio walimweleza mwandishi wa habari hizi kuwa polisi walipofika waliwasihi wananchi kutawanyika kwa kuwa ungo na tunguri zake zilikuwa zimeteketezwa kwa moto na diwani huyo mbele ya wananchi hao.
“Wananchi waliendelea kupinga na kudai ndani ya nyumba kuna rubani na abiria wa ndege nimewahifadhi…polisi wakawachagua wananchi watano na kuingia ndani ya nyumba kuwasaka watu hao…hawakuona kitu, walitoka nje na kuwamabia wenzao hata hivyo wenzao walibisha” alisema Chehako alihojiwa nyumbani kwake.
Aliongeza kuwa “walianza kurusha mawe nyumba…polisi walianza kupambana nao kwa kuwarushia mabomu…hata hivyo wananchi walikuwa wanakimbia na kwenda upande wapili kufanya vurugu”
Akihadithia mkasa huo, Chihako alibainisha kuwa ni kawada yake kuamka alfajiri kwa ajili ya sala ya asubuhi, lakini asubuhi ya jana alishindwa kuamka mapema, hata hivyo hakuweza kuhisi jambo lolote.
“Ilipofika saa 12 asubuhi nikaanza kusikia watu wakishangaa kitu nje, nilipotoka nikakuta nyungo na tunguri ndani yake…mara wakaja vijana wawili na pikipiki wakachukua ule ungo na kukimbia nao…nikawatuma vijana wawafuate waurudishe…walifanikiwa na nyungo ile ilirejeshwa nyumbani hapa na ndipo nilipouteketeza kwa moto” alisema na kuongeza kuwa
Nilidhani yatakuwa yameisha, lakini wananchi waliendelea kudai nimewafungia wahuska ndani, si kweli hakuna mtu humu ndani wala mimi sijui kilichotokea hadi hivyo vitu vikawa humu ndani”
Katika mapambano hayo ya wananchi na polisi, wananchi kwa kutumia mawe wamemjeruhi Mwandishi wa Habari wa Channel Ten mkoani hapa, John Kasembe kwa jiwe kichwani, sehemu za kisogoni ambapo ametibiwa zahanati ya Fajima na anaendelea vizuri.
Kwa mujibu wa Kasembe alipigwa mawe kichwani akiwa kazini kukusanya habari na wananchi waliokuwa wakiwarushia mawe polisi.
Ofisa wa polisi ambaye jina lake hakutaka litajwe kwa sababu si msemaji wa jeshi hilo amethibitisha kutokea kwa tuki hilo na kuongeza kuwa gari moja ya polisi PT 1421 limevunjwa kioo cha mbele kwa mawe.
Hadi saa 12.00 jioni bado polisi walikuwa wanaendelea kupiga mabomu ya machozi hewani huku wananchi wakionekana kujipanga katika makundi hali iliyotishia usalama wa maeneo hayo.
katika vurugu hizo nyumba ya mbunge wa mtwara vijijini Hawa Ghasia na ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa mtwra Mohamed Sinani, pamoja na Mahakama ya mwanzo vimechomwa moto.
Na huko masasi habari ambazo zimetufikia hivi punde kutoka eneo la tukio Nyumba ya Mbunge pamoja na Ofisi za Halmashauri zimechomwa moto na vurugu bado zinaendele, na chanzo cha fujo hizo bado hakijafahamika.
Picha kwa hisani ya Abdalah Nasoro
No comments:
Post a Comment