Tuesday, January 1, 2013



Kundi A: Kipa Bora
Mwandini Ally- Azam FC, Juma Kaseja- Simba, Shaaban Kado- Mtibwa Sugar, Ally Mustapha-Yanga, Jackson Chove-Coastal Union, Deogratius Munishi- Azam FC

Kundi B: Beki Bora
 Nassor Said – Simba, Nadir Haroub – Yanga, Agrey Morris- Azam FC, Amir Maftah- Simba, Kelvin Yondan-Yanga  na Shomari Kapombe-Simba.

Kundi C: Kiungo Bora
Shaban Nditi –Mtibwa, Frank Domayo- Yanga, Mwinyi Kazimoto-Simba, Amri Kiemba-Simba, Chande Mgoja- Mgambo JKT na Abubakar Salum-Azam FC.

Kundi D: Mshambuliaji Bora
John Bocco – Azam FC, Mrisho Ngassa – Simba, Hussein Javu -Mtibwa FC, Amiry Omary-JKT Oljoro, Simon Msuva-Yanga, Nsa Job-Coastal Union.

Kundi E: Mchezaji anayechipukia
Mudasir Yahya-Azam FC, Ramadhan Singano-Simba, Edward Christopher-Simba, Manyika Peter Manyika- Mgambo JKT, Miraji Adam-Simba na Chande Mgoja- Mgambo JKT

 Kundi F: Mchezaji Bora wa Kike
Ester Chabruma-Sayari Queens, Mwanahamisi Omar-Mburahati Queens, Mwapewa Mtumwa-Ever Green, Fatuma Mustafa-Sayari Queens, Asha Rashid-Mburahati Queens na Sophia Mwasikili-Luleburgaz Spor Kulubu- Uturuki.

Kundi G: Mchezaji Bora wa mwaka 2012
Mchezaji atakayetwaa tuzo hii atatoka katika makundi yaliyotajwa hapo juu hii ikiwa na maana kwamba kuanzia kundi A-E. hii ni kumaanisha kuwa wanawake hawataingia kwenye kundi hili wala kwa sababu tayari wanayio tuzo yao tayari kama inavyoonekana katika kipengele F.

Kundi H: Mchezaji Bora Kigeni
Haruna Niyonzima-Yanga, Kipre Tchetche-Azam FC, Emmanuel Okwi-Simba,  Felix Sunzu-Simba, Hamis Kiiza-Yanga na Jerry Santo-Coastal Union.

TUZO ZA HESHIMA
Kundi I: Mchezaji bora wa zamani
Madaraka Suleiman – Simba, Edibily Lunyamila-Yanga/Simba/Twiga FC,
Mohamed Mwameja-Simba, Yusuf Macho-Simba/Kagera Sugar, Zamoyoni Mogela-Simba/Yanga na Kenny Mkapa-Yanga.

Kundi J: Maendeleo soka la Wanawake (tuzo mbili Mwanamke na Mwanaume)
Stephania Kubumba-Sayari, Arafa Tamba-Mburahati Queens, Fatma Makambara-Sayari, Pili Kambangwa- Mchangani, Joha Halfan-Vijana Queens, Amin Bakhresa, Frenk Mchaki na Idd Azan.

 Kundi K:Mwanasiasa wa Afrika aliyesadia maendeleo ya michezo
Benjamin Mkapa-Tanzania, Daniel Arap Moi-Kenya na Joachim Chisano-Msumbiji
 Katika kipengere hiki ni kwamba kilichoangaliwa ni namna gani mwanasiasa mstaafu alivyweza kusaidia michezo kwa ujumla ikiwemo soka. Hapa inaangaliwa ujewekaji wa miundo mbinu, kama ujezi wa viwanja vya michezo, mafanikio katika klabu na  timu za taifa katika nchi ambayo amekuwa akiiongoza.
 Pia kipengere hiki pia kinaangalia katika kipindi kisichozidi miaka 10 ya utawala akiwa kama mkuu wa nchi husika.
 Baada ya kufuatilia kwa takriban mwaka mmoja katika nchi zilizopo jirani na Tanzania, imeonekana wazi kuwa viongozi hao wastaafu ndiyo wenye waliofikia viwango ambavyo kamati ilivihitaji.

Kamati ya maandalizi ya Fainali ya tuzo hiyo ya Mwanasoka Bora wa mwaka (Wazalendo Footballer of the Year), iliamua kusogezwa mbele kwa fainali hizo ambazo zilikuwa zifanyike Desemba 30 mwaka 2012 jijini Dar es Salaam ambapo sasa zitafanyika Januari 31 mwaka 2013.
Licha ya hatua muhimu kukamilika lakini zipo sababu za msingi ambazo kamati imeona ni busara kuzifuatilia ili kufanya tuzo hizo kufanyika kwa ufanisi.
  1. Asilimia 90 (90%) ya Wajumbe wa kamati hiyo ni wanachama wa chama cha makocha wa Tanzania (Tafca) ambao wapo kwenye mchakato wa uchaguzi mkuu wa chama chao hivyo kushindwa kukamilisha baadhi ya mambo kwa wakati.
  1. Pia wapi baadhi ya wageni muhimu ambao walialikwa asilimia (80%) wameonyesha kutokuwepo kwa tarehe hiyo (Desemba 30, 2012) kwa sababu watakuwa nje ya jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya siku kuu za mwisho wa mwaka jambo ambalo kamati imeona pia ni jambo la msingi.
Kwa kuzingatia uzito wa jambo lenyewe kamati iliona ni busara kusogeza mbele kwa siku 30 kwa lengo la kuwapa nafasi wahusika kwa pande zote mbili kuendelea na matayarisho hayo ili kuwa na ufanisi kwenye jambo hili la kitaifa lenye nia ya kusaidia kuinua na kuendeleza vipaji vya soka kwa Watanzania.

No comments: