Friday, January 18, 2013

50 WAREJESHA FOMU KUWANIA UONGOZI TFF,KATI YA WATU 52 WALI00MBA
WANAMICHEZO 50 kati ya 52 waliochukua fomu kuomba kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) utakaofanyika Februari 24 mwaka huu wamerejesha fomu hizo.

Waombaji ambao hawakurejesha fomu ni Geofrey Nyange aliyekuwa akiomba ujumbe wa Kamati ya Utendaji kuwakilisha mikoa ya Morogoro na Pwani, na Shufaa Jumanne aliyekuwa akiomba kuwakilisha Kanda ya Dar es Salaam.

Orodha kamili ya waombaji ambao wamerejesha fomu ni Athuman Nyamlani, Jamal Malinzi, Omari Nkwarulo na Richard Rukambura (Rais).

Michael Wambura, Ramadhan Nassib na Wallace Karia (Makamu wa Rais).

Kwa upande wa ujumbe wa Kamati ya Utendaji ni Abdallah Musa, Salum Chama na Kaliro Samson (Kagera na Geita), Jumbe Magati, Mugisha Galibona, Richard Rukambura, Samuel Nyalla, Titus Osoro na Vedastus Lufano (Mara na Mwanza).

Epaphra Swai na Mbasha Matutu (Shinyanga na Simiyu), Charles Mugondo, Elly Mbise na Omari Walii (Arusha na Manyara), Ahmed Mgoyi na Yusuph Kitumbo (Kigoma na Tabora), Ayubu Nyaulingo, Blassy Kiondo, Nazarius Kilungeja na Selemani Kameya (Katavi na Rukwa) na James Mhagama na Stanley Lugenge (Njombe na Ruvuma).

Athuman Kambi, Francis Ndulane na Zafarani Damoder (Lindi na Mtwara), Hussein Mwamba na Stewart Masima (Dodoma na Singida), Farid Nahdi, Hassan Othman Hassanoo, Riziki Majala na Twahili Njoki (Morogoro na Pwani), David Lugenge, Elias Mwanjala, Eliud Mvella na John Kiteve (Iringa na Mbeya), Davis Mosha, Khalid Mohamed na Kusiaga Kiata (Kilimanjaro na Tanga) na Alex Kamuzelya, Juma Pinto, Muhsin Balhabou, Omari Abdulkadir na Shaffih Dauda (Dar es Salaam).

Wakati huo huo: Waombaji wote sita wa uongozi katika Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board) ambayo uchaguzi wake utafanyika Februari 22 mwaka huu wamerejesha fomu.

Kwa upande wa Mwenyekiti waombaji ni Hamad Yahya wa Kagera Sugar na Yusuph Manji wa Yanga wakati Makamu Mwenyekiti aliyeomba ni Said Mohamed wa Azam.

Nafasi mbili za ujumbe wa Bodi ya Ligi Kuu kwa klabu za Daraja la Kwanza zimeombwa na watu watatu. Waombaji hao ni Christopher Peter Lunkonde wa Moro United, Kazimoto Miraji Muzo wa Pamba ya Mwanza na Omari Khatibu Mwindadi.

Kamati ya Uchaguzi ya TFF itaanza kukutana kesho kwa ajili ya kupitia fomu zote zilizowasilishwa na waombaji kwa ajili ya uchaguzi wa TFF na ule wa Bodi ya Ligi Kuu.

Pia Kamati inapenda kuwakumbusha waombaji uongozi kuzingatia Kanuni za Uchaguzi, kwani baadhi yao wameanza kufanya kampeni kupitia vyombo vya habari. Kwa walioanza kufanya kampeni kabla ya wakati wanajiweka katika hatari ya kuenguliwa kushiriki katika uchaguzi.

Na Boniface Wambura
WANAMICHEZO 45 wamechukua fomu kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) utakaofanyika Februari 24 mwaka huu. Nafasi zinazowaniwa ni Rais, Makamu wa Rais na wajumbe wa Kamati ya Utendaji kuwakilisha kanda 13 tofauti.
Waombaji wapya 11 waliojitokeza leo (Januari 18 mwaka huu) ni Richard Rukambura anayeomba urais wakati kwa upande wa ujumbe wa Kamati ya Utendaji ni Kaliro Samson, Jumbe Magati, Richard Rukambura, Omari Walii, Ahmed Mgoyi, John Kiteve, Stanley Lugenge, Francis Ndulane, Riziki Majara na Hassan Othuman Hassanoo.
Mwisho wa kuchukua fomu kwa waombaji wote ni leo (Januari 18 mwaka huu) saa 10 kamili alasiri. Fomu pia zinaweza kuchukuliwa katika tovuti ya TFF ambayo ni www.tff.or.tz na kurejeshwa kupitia email ya tfftz@yahoo.com Pia Kanuni za Uchaguzi za TFF zinapatikana katika tovuti hiyo.
Orodha kamili ya waombaji ni Athuman Nyamlani, Jamal Malinzi, Omari Nkwarulo na Richard Rukambura (Rais). Walioomba kuwania nafasi ya Makamu wa Rais ni Michael Wambura, Ramadhan Nassib na Wallace Karia.
Kwa upande wa ujumbe wa Kamati ya Utendaji ni Salum Chama na Kaliro Samson (Kagera na Geita), Jumbe Magati, Mugisha Galibona, Richard Rukambura, Samuel Nyalla, Titus Osoro na Vedastus Lufano (Mara na Mwanza).
Epaphra Swai na Mbasha Matutu (Shinyanga na Simiyu), Charles Mugondo, Elly Mbise na Omari Walii (Arusha na Manyara), Ahmed Mgoyi na Yusuph Kitumbo (Kigoma na Tabora), Ayubu Nyaulingo, Blassy Kiondo, Nazarius Kilungeja na Selemani Kameya (Katavi na Rukwa) na James Mhagama na Stanley Lugenge (Njombe na Ruvuma).
Athuman Kambi, Francis Ndulane na Zafarani Damoder (Lindi na Mtwara), Hussein Mwamba na Stewart Masima (Dodoma na Singida), Farid Nahdi, Geofrey Nyange, Hassan Othman Hassanoo, Riziki Majara na Twahili Njoki (Morogoro na Pwani), Elias Mwanjala, Eliud Mvella na John Kiteve (Iringa na Mbeya), Khalid Mohamed (Kilimanjaro na Tanga) na Muhsin Balhabou, Omari Abdulkadir na Shaffih Dauda (Dar es Salaam).
WAOMBAJI WATATU WAPYA WAMEJITOSA KATIKA KINYANG’ANYIRO CHA KUWANIA UONGOZI WA BODI YA LIGI KUU (TPL BOARD)

WAOMBAJI watatu wapya wamejitosa katika kinyang’anyiro cha kuwania uongozi wa Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board) ambayo uchaguzi wake utafanyika Februari 22 mwaka huu.
Walioingia leo (Januari 18 mwaka huu) kwenye kinyang’anyiro hicho ni Hamad Yahya wa Kagera Sugar anayeomba uenyekiti wakati Christopher Peter wa Moro United na Kazimoto Miraji Muzo wa Pamba ya Mwanza wanaoomba ujumbe wa Bodi kuwakilisha klabu za Ligi Daraja la Kwanza.
Orodha kamili ya waombaji uongozi wa Bodi ya Ligi Kuu ni Hamad Yahya wa Kagera Sugar na Yusuf Manji wa Yanga wanaoomba uenyekiti wakati Makamu Mwenyekiti aliyeomba ni Said Mohamed wa Azam.
Kwa upande wa wajumbe wawili kuwakilisha klabu za Daraja la Kwanza ni  Christopher Peter Lunkombe wa Moro United ya Dar es Salaam na Kazimoto Miraji Muzo wa Pamba ya Mwanza


MAREFA kutoka Afrika Kusini ndiyo watakaochezesha mechi ya kwanza ya raundi ya awali ya Ligi ya Mabingwa kati ya Simba ya Tanzania na Clube Recreation Libolo ya Angola itakayofanyika Februari 17 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Waamuzi hao ni Daniel Volgraaff atakayepuliza filimbi wakati wasaidizi wake ni Enock Molefe, Lindikhaya Bolo na Lwandile Mfiki. Kamishna wa mechi hiyo atakuwa Emmanuel Lesita kutoka Lesotho.
Aidha, Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limewateua Watanzania Leslie Liunda na Alfred Rwiza kuwa makamishna wa mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika zinazoanza mwezi ujao.
Rwiza ameteuliwa kuwa kamishna wa mechi kati ya APR ya Rwanda na Vital’O ya Burundi itakayochezwa nchini Rwanda kati ya Februari 15 na 17 mwaka huu.
Naye Liunda atakuwa kamishna wa mechi ya marudiano kati ya Tusker ya Kenya na St. Michel United ya Seychelles itakayochezwa Kenya kati ya Machi 1 na 3 mwaka huu. Mechi zote ni za raundi ya awali.
Wakati huo huo: Waamuzi wanne wa Tanzania wameteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kuchezesha mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa kati ya URA ya Uganda na Cotton Sport ya Cameroon itakayochezwa jijini Kampala kati ya Machi 1 na 3 mwaka huu.
Orden Mbaga ndiye atakayekuwa mwamuzi wa kati na atasaidiwa na mwamuzi msaidizi namba moja Jesse Erasmo wakati mwamuzi msaidizi namba mbili ni Hamis Chang’walu. Mwamuzi wa mezani ni Israel Mujuni na Kamishna wa mechi hiyo atakuwa Souleiman Waberi wa Djibouti.

No comments: