![]() |
Hamisi keiza na Meneja wa yanga uwanja wa ndege wa istanbul wakisubiri ndege nyingine |
![]() |
Wachezaji wa Yanga wakiwa wamepumzika katika Uwanja wa ndege wa kimataifa Instambul wakisubiria ndege ya kwenda katika mji wa Antalya Wakipata menu |
Young Africans imefikia katika hoteli ya Fame Residence Lara & Spa kilomita chache kutoka katika uwanja wa ndege wa antalya, ambapo hoteli ya Fame Residence ipo mwambaoni mwa bahari ya mediteranian.
Mwanzoni Yanga ilikuwa ifikie katika hotel ya Sueno Beach Hotel iliyopo kilometa 70 kutoka uwanja wa ndege lakini jana siku moja kabla ya safari ilifanya mabadiliko na kuamua kuhamia katika hotel ya Fame Residence.
Wachezaji wamefurahi mandhari ya hotel kwani ni miongoni mwa hotel za nyota tano katika mjii huu wa Antalya hivyo wamefariijika na kuupa hongera uongozi kwa hatua waliyofikia ya kukubaliana na mwalimu kuweka kambi ya mafunzo nchini Uturuki.
Timu itaanza mazoezi leo asubuhi katika viwanja vilivyopo katika eneo la hotel ya fame, ambapo kwa siku timu itakua inafanya mazoezi mara mbili kwa siku asubuhi na jioni.
Kuhusu hali ya hewa ni baridi kiasi na sio baridi kali kama ilivyokuwa inatangazwa na vyombo vya habari hapo awali.
Chanzo www.youngafricans.co.tz
No comments:
Post a Comment