Saturday, December 22, 2012

STARS WAZIMA RISASI ZA SHABA UWANJA WA TAIFA YAITANDIKA  BINGWA WA AFRIKA ZAMBIA 1-0

Mrisho Ngasa na wachezaji wenzake wakishangilia bao.

TIMU ya taifa ya tanzania taifa stars leo imewatoa kimasomaso watanzania baada ya kuibanjua timu ya taifa ya Zambia chipolopolo goli moja kwa bila,Goli pekee lilofungwa na mchezaji Mrisho Ngassa katika dakika ya 45 katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki.

Timu zote ambazo zilikuwa zimewakosa wachezaji wao muhimu ziliuanza mchezo wa vizuri huku Stars ikionekana kucheza vizuri kwenye upande wa ulinzi na safu ya kiungo.

Tanzania iliishambulia sana Zambia katika kipindi cha kwanza  kabla ya dakika 45 mrisho ngasa kupokea pasi nzuri kutoka kwa Mwinyi Kazimoto na kufumua shuti kali na kuiandikia bao safi Tanzania hivyo kwenda mapumziko wakiwa kifua mbele kwa 1-0.

Kipindi cha pili Zambia walirudi kwa kasi wakiingiza baadhi ya silaha zao walizoziacha nje mwanzoni lakini bado walishindwa kuipita ngome imara ya ulinzi ya stars

Hadi kipenga cha mwisho kinapulizwa matokeo yakiwa 1-0 kwa bila, Stars ikitoka na ushindi mzuri iliyostahili kwa kucheza soka safi kabisa na la kuridhisha.

No comments: