Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete leo ameupokea uongozi klabu ya Sanderland ya nchini England ambao umetua hapa nchini kwa safari za kitalii lakini pia ukiwa na lengo la kuwekeza katika soka hla vijana.
Uongozi huo wa Sunderland umesema kuwa baada ya kukutana na balozi wa Tanzania nchini humo na kuzungumza nae kuhusu swala la uwezekezaji Mwenyekiti wa klabu hiyo ameona bora waje kuonana na Viongozi wakuu wa nchi hasa baada ya Tanzania kudhamini ligi kuu ya Uingereza kwa kupitisha mabangombalimbali yahusuyo utalii katika ligi hiyo ,
Aidha Rais kikwete amemsifu balozi wa Tanzania Nchini Uingereza kwa kazi walioyofanya na Waziri wa utalii Mh kagasheki kwani wamefanya kazi nzuri zaidi kipindi hiki .
Kwa upande mwingine baadhi ya wachezaji watapa mafunzo ya kwenda sunderland hasa wenye umri mdogo zaidi
Viongozi hao wa sunderland wamesema kitu kikubwa watakachofanya ni kuendeleza michezo katika sekta ya uongozi na kutazama namna ya kutoa mafunzo kwa wachezaji na viongozi wa soka hasa katika swala la menejiment ambalo ndilo eneo lenye udhaifu zaidi katika michezo ,
kwa upande mwingine Rais alimwalika Mh Aden Rage mwenyekiti wa klabu ya soka simba ambao zamani walikuwa wakitumia hilo kabla ya kubadili kuitwa simba naibu waziri wa michezo fenela mukangara amesema kuwa hii ni faida ya kwanza ambayo tanzania inapata baada ya kutangaza katika ligi hiyo na waanaamini fursa zaidi zitajitokeza katika kutangaza katika ligi hyo.
No comments:
Post a Comment