Friday, December 21, 2012

MAKOCHA WA STARS NA CHIPOLOPOLO WAZUNGUMZA NA VYOMBO VYA  HABARI JUU YA MCHEZO WA KESHO

Makocha Kim Poulsen wa Tanzania (Taifa Stars) na kocha msaidizi wa Zambia (Chipolopolo) PATRIC BONELE wamezungumza na waandishi wa habari juu ya  pambano lao litakalochezwa kesho Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kocha wa stars Kim polsen amesema stars itapata nafasi nzuri ya kujifunza kwa kucheza na mabingwa hao wa afrika ambao pia wamechaguliwa kuwa timu bora ya afrika kwa mwaka huu.
Naye kocha msaidizi wa chipolopola Patick Bondele amesema wanaichukulia mechi hiyo kwa umuhimu kwa vile hawaifahamu vizuri Stars.
Kwa upande wake nahodha wa zambia Christopher Katongo, ambaye pia ni Mwanasoka Bora wa Afrika wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) mwaka huu, amesema hawana pressure kuelekea mchezo huo ingawa hawaifahamu Tanzania.
Naye nahodha wa stars Juma kaseja amewaomba watanzania kuipa sapoti timu yao hapo kesho.
Kwa upande wake katibu mkuu wa TFF Angetile Osiya ametoa wito kwa mashabiki kuwapa moyo wachezaji  Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu ambao hawatacheza mchezo huo kutokana na majeruhi.

No comments: