Sunday, December 30, 2012

LAMPARD APIGA 2 KUIPAISHA CHELSEA HADI NAFASI YA TATU KATIKA MSIMAMO WA LIGI KUU YA ENGLAND NI BAADA YA USHINDI WA 2-1 DHIDI YA EVERTON.

LONDON, England
FRANK Lampard alionyesha thamani yake kwa  Chelsea baada ya kufunga magoli mawili ‘makali’ yaliyoipa ushindi wa ugenini wa mabao 2-1 dhidi ya Everton leo na kukwea hadi katika nafasi yake ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England. 

Huku kukiwa na uvumi mwingi kuhusiana na hatma yake ndani ya Chelsea, alionyesha kiwango cha juu na kufunga mabao yote huku goli la Everton likifungwa na Steven Pienaar. 

Ushindi wan ne mfululizo wa Chelsea chini ya kocha Rafael Benitez umeiinua hadi kubakiza pointi nne tu kabla ya kuifikia Manchester City inayoshika nafasi ya pili, huku Chelsea ikiwa na mechi moja mkononi.

No comments: