CHEKA ATAMBA KUMCHAKAZA CHIMWEMWE WA MALAWI, ASEMA HATA YEYE NI MJESHI KAMA CHIMWEMWE
Check this out on Chirbit
Bondia Francis Cheka ambaye ni bingwa wa mikanda mingi pamoja na IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki wa uzito wa kati, amesema amejiandaa kumchakaza bondia Chiotra Chimwemwe wa Malawi.
Katika pambano wa raundi 12 kuwania ubingwa wa IBF Afrika, cheaka ametamba kumwonyesha mwanajeshi huo wa jeshi la Malawi jinsi ngumi zinavyotakiwa kuchezwa kwani hata yeye ni mjeshi.
Cheka ametamba kuwa ataubakiza mkanda huo hapa Tanzania kwani ndipo mahala unapostahili kukaa!
Bondia Chimemwe Chiotra ni mwanajeshi kutoka katika jeshi la Malawi na alianza harakati zake katika ngumi za kulipwa mapema kabisa na kujizolea sifa kemkem ambazo zimemwezesha kukubaliwa na IBF kugombea mkanda wake.
Mabondia hao kesho watapima uzito na afya kwenye Ukumbi wa Tripple A, kabla ya pambano lao siku inayofuata kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.
Tayari mabondia wote wamekwishawasili Arusha tangu wiki iliyopita licha ya kila mmoja kukwepa kuonana na mwenzake na kesho watakutana kwa mara ya kwanza wakati wa kupima uzito.
Chimwemwe aliingia katika jiji la Arusha kwa mbembwe tarehe 20 akifuatana na kocha wake Daudi Kikwanje na kudai kuwa wamekuja kuuchukua mkanda huo wa IBF waupeleka nchini Malawi ambako ndipo unapostahili kukaa.
Ikumbukwe kwamba Mpambano huo wa kugombea ubingwa wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati utafanyika wakati kukiwa na mzozo wa mpaka wa ziwa Nyasa kati mya Tanzania na Malawi.
Mpambano huo unaowakutanisha Mtanzania Francis Cheka na Mmalawi Chimwemwe Chiotra unategemea kujenga uhusiano kati ya nchi hizi mbili zenye mahusiano ya muda mrefu.
IBF imewateua Onesmo Ngowi kuwa msimamizi mkuu akisaidiwa na Nemes Kavishe(Refarii), Boiniface Wambura (Jaji), Mark Hatia (Jaji) na Galous Lingongo kutoka jiji la Tanga kama jaji.
No comments:
Post a Comment